Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wa Nyamazobe watatuliwa changamoto ya barabara

ROAD.jpeg Wananchi wa Nyamazobe watatuliwa changamoto ya barabara

Thu, 11 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi wa Mtaa wa Nyamazobe Kata ya Mkolani wilayani Nyamagana mkoani Mwanza waliokuwa hawana sehemu ya kupita kufuatia mtaa wao kutokuwa na barabara, hatimae Serikali imekamilisha ujenzi wa barabara ya kilometa 2.38 katika eneo hilo.

Wakizungumza jana wakati wa ziara ya kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo ya utekelezaji wa miradi ya barabara inayosimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA)na ujenzi wa daraja la Fumagila Jiji la Mwanza.

Mkuu wa Wilaya hiyo Dk.Phillis Nyimbi, wameishukuru Serikali kwa kujenga barabara hiyo ya Nyamazobe-Kasese Nyahingi itakayo rahisisha usafiri wakati wa kupata huduma mbalimbali ikiwemo mahitaji ya chakula, huduma za afya na kuwawezesha wanafunzi kufika shule kwa wakati.

Amesema kwa sasa wananchi wanapata usafiri kwani mawasiliano siyo jambo dogo na barabara hiyo ni ya kihistoria ambayo itafanya kuendelea kumkumbuka sana Rais kwa maagizo yake ya barabara hiyo ijengwe na ifunguke ili wananchi wasipate shida hivyo aliwataka wakazi wa maeneo hayo kuitunza kuitumia katika uzalishaji mali na kuilinda kwani ni ya kwao.

"Eneo hilo ni la kihistoria kwani lilikua alifikiki na wananchi walikuwa wanapanda kwenye miamba na sisi wenyewe ni mashahidi viongozi tulifika hapa tukapanda kwenye miamba kufuatilia hiki ambacho wananchi walikianzisha kama alivyosema Meneja wa TARURA 2018."

"Wananchi hawa wa Nyamazobe walikaa kwenye mkutano wao wakaadhimia kuanzisha barabara kutokana na adha waliokuwa wanaipata na walivyoanza tukio lile Rais aliliona hilo na kutoa fedha kwa kumtuma Waziri wa TAMISEMI Seleman Jafo ambaye alikuja akiwa amebeba taslimu milioni 20, kikubwa tunasema tunamshukuru sana Rais kwa barabara hii aliotupatia ya kihistoria ambayo imeleta maendeleo kwa wananchi wetu tumeshuhudia maduka mapya,magari na pikipiki zinapita hapa wananchi wanapata huduma ya usafiri kwani mawasiliano siyo jambo dogo," amesema Dk.Nyimbi.

Ziara ya Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Nyamagana katika utekelezaji wa miradi ya maji imezungukia mradi wa daraja la Fumagila ambao kwa sasa umefikia asilimia 70 ya utekelezaji wake kwa kujenga misingi minne ya daraja na kunyanyua nguzo nne ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi wa sita mwaka huu, mradi wa Barabara Nyamazobe -Kasese-Nyahingi ambao umekamilika na wananchi wameanza kuitumia na matengenezo ya kazi za dharura daraja la Nyegezi stendi - Malimbe uharibifu katika daraja hilo ulitokana na mvua za vuli na masika.

Mmoja wa wakazi wa mtaa wa Nyamazobe ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne, Junior Laurent, ameishukuru Serikali kupitia Rais Magufuli kwa kuwasaidia kupatikana kwa barabara hiyo kwani awali walikuwa wanapata changamoto wakati wa kwenda shuleni kwa kulazimika kupanda juu ya miamba na wakati mwingine kuanguka.

"Tumefurahi sana na tunamshukuru Rais wetu ametuletea maendeleo mazuri na ametusaidia kwa sababu zamani tulikuwa tunasumbuka sana kwenda shule tunapita kwenye mawe, tulikua tukichota maji tunaruka mawe ila sasa hivi tunavuka tu barabara,tunaweza kuletwa na bodaboda ukashuka tu hapo na kuingia ndani bila usumbufu,"amesema Laurent.

Mmoja wa wananchi waliojitolea kupisha ujenzi huo, Faustina Selestine, mkazi wa Nyamazobe, anasema, awali kulikua hakuna njia wala barabara mbayo inapitika kihurahisi hali iliyowapa wakati mgumu hata wakati wa kutaka kusafirisha maiti iliwalazimu kubeba mpaka chini tena kwa kupita juu ya mawe na wakitaka kuleta vifaa vya ujenzi ili kuwa shida maana walilazimika kutumia watu kubeba na kuwafikishia eneo husika hali iliyopelekea kufanya gharama kuwa kubwa.

"Nilitoa eneo ili kuleta chachu ya maendeleo hii barabara watatumia watu wengi ata vizazi vijanyo huu ni uzalendo unapoona kuna changamoto na uwezo wa kutatua upo ni vyema ukafanya hivyo pasipo kuangalia faida sasa tunaitumia barabara hii kwa faida " amesema

Kwa upande wake Meneja TARURA Jiji la Mwanza, Mhandisi Mohamed Muanda, anasema mradi wa ujenzi huo sehemu kubwa uanzishwaji wake umetokana na juhudi za wananchi wa mtaa huo kwa kuungana na kuchangia fedha kwa ajili ya kupasua mawe ili kujenga barabara hiyo kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Rais za kuleta nchi maendeleo.

Amesema Rais aliunga mkono jitihada za wananchi wa mtaa huo kwa kuchangia milioni 20, ambapo TARURA iliamua kuingiza barabara hiyo katika mpango kazi wa mwaka wa fedha wa 2018/19,ambapo mpaka sasa mradi huo umekamilika kwa asilimia 100 uliohusisha ujenzi wa mitaro,makalavati,uchongaji wa barabara na uwekaji wa changarawe, barabara ya mawe na zege pamoja na upasuaji mkubwa wa miamba uliogharimu zaidi ya milioni 573.8(573,819,527.19) kwa fedha za Serikali kupitia wao,ulioanza Desemba 4,2018 na kukamilika Aprili 30 mwaka 2019.

Amesema wamejenga barabara ya mawe yenye urefu wa mita 140 huku ya zenge ikiwa mita 538 iliyojengwa kwenye mlima mkali,ambapo sehemu iliyo baki ya karibu kilomita 1.6 ni kwa kiwango cha changarawe ambapo wataweka kwenye bajeti huku wakiendelea kutafuta ela ili nayo wajenge kwa kiwango cha mawe na kufanya barabara hiyo yote yenye urefu wa kilomita 2.38 kuwa ya kiwango cha mawe na zege.

"Changamoto ilikuwa ni upasuaji wa miamba ambayo ilikuwa ni mikubwa yenye urefu wa mita 3 hadi 7 kwenda juu na upana wa mita 4 hadi 6, tulikaa na viongozi wa mitaa kupitia vikao vyao tukakubaliana milioni 20 ianze kazi ya kupasua miamba ambayo watu wa madini walitusaidia kwa kuingia makubaliano na mtaa na kati ya hizo fedha zilitumika milioni 17 na kubaki milioni 3 ambapo zipo kwenye akaunti ya Serikali ya mtaa,nimewaambia zibaki na pale greda( tingatinga) lao litakapo tengemaa fedha hizo zitumike kuchongea barabara za Kata ya Mkolani na mitaa yake," anasema Mhandisi Muanda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live