Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi kicheko shule ikikabidhiwa kwa DC baada ya kukarabatiwa

Fri, 13 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Simanjiro. Taasisi isiyo ya Serikali ya ECLAT Foundation la Emboreet Wilayani Simanjiro mkoani Manyara kwa kushirikiana na Upendo Society la Ujerumani wamekamilisha ujenzi wa miundombinu ya shule ya msingi Kimelok.

Shule hiyo iliyopo kijiji cha Kimotorok kata ya Loiborsiret imejengwa kwa Sh267 milioni.

Wananchi wa kijiji cha Kimotorok waliomuomba mwenyekiti wa ECLAT Foundation kuikarabati kwani miundombinu yake ilikuwa mibovu.

Miradi hiyo imekabidhiwa serikalini kupitia kwa mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Zephania Chaula.

Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Peter Toima amesema shirika hilo limekuwa msaada kwa jamii katika sekta ya elimu, afya na kuwezesha kiuchumi vikundi vya maendeleo.

Toima amesema baada ya kuikabidhi Serikali shule pia watakabidhi shule ya msingi Nadoilchukin ya Komolo wilayani Simanjiro na Lengijape ya Lorkisalie wilayani Monduli baada ya kuzikamilisha.

Pia Soma

Advertisement
"Tunasaidiana na Serikali katika kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuhakikisha jamii inanufaika kwa namna moja au nyingine," amesema Toima.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kimotorok akiwemo, Paschal Shinini wameipongeza taasisi hiyo kwa kufanikisha ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz