Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi Vunjo kunufaika na maji safi

47a5e8482eebb2c9a1d55e3025a89173 Wananchi Vunjo kunufaika na maji safi

Thu, 14 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Charles Kimei amesema wananchi wataanza kupata huduma ya maji safi na salama baada ya Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) kumaliza kufanya tathimini ya upatikanaji wa maji jimboni humo.

Kimei amebainisha hayo jana jimboni humo mkoani Kilimanjaro ambapo ametaja kata zitakazonufaika baada ya kufanyika tathimini ni Kilema Kaskazini, Kilema Kusini na maeneo ya ukanda wa tambarare.

“ Muda sio mrefu wananchi mtaanza kupata huduma ya uhakika ya maji baada ya upembuzi yakinifu kukamilika kwakuwa tatizo la maji limekuwa kero kwenu kwa kipindi kirefu licha ya kuwepo vyanzo vingi vya maji katika maeneo haya” amesema Kimei.

Chanzo: habarileo.co.tz