Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi Uyui walalama ahadi ya maji kushindwa kutekelezwa kwa miaka Tisa

82804 Pic+maji Wananchi Uyui walalama ahadi ya maji kushindwa kutekelezwa kwa miaka Tisa

Tue, 5 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Wakazi wa Kata ya Kigwa wilayani Uyui, wamelalamikia udanganyifu uliofanywa na Serikali kutatua tatizo la maji kwenye kata yao.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara,mkazi wa kijiji cha Kigwa, Dotto Kilimila amesema mwaka 2010 wakati Waziri Mkuu akiwa Mizengo Pinda,waliahidiwa maji ambayo yalitoka kwa muda wa siku. Mbili au tatu.

Amesema walioahidiwa maji baada ya kulalamikia tatizo kubwa la maji na kuambiwa litatatuliwa katika kipindi cha muda mfupi.

"Baada ya kuondoka Waziri mkuu,tuliona maji yakitoka katika tanki hilo unaloliona hapo mbele yako muda wa siku kama mbili au tatu na kukauka" Amesema na baadhi ya watu kushangilia.

Hata hivyo Dotto amesema ana imani na Waziri Mbarawa na Serikali ya awamu ya tano kuwa haitadanganya kama walivyodanganywa miaka tisa iliyopita,akisema Serikali iliyopo ni ya vitendo.

Akijibu baada ya kusikiliza baadhi ya wakazi wa kata hiyo,alisema atahakikisha wakazi wa kata hiyo,wanapata maji safi na salama katika kipindi kifupi kijacho.

Ameagiza wataalamu kufanya tathmini ya gharama kutoka bomba kuu la mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria na kwamba Serikali itagharamia.

"Hata kama zitakuwa shilingi bilioni kumi na mbili au chini ya hapo,Serikali itagharamia" Amesema

Amewaeleza kuwa yeye na Serikali hii,hawezi kuwadanganya wananchi na kwamba wasubiri maji muda mfupi ujao.

Amesema Serikali imetoa maji zaidi ya km 200 kutoka Shinyanga kuja Tabora na kwamba haiwezi kushindwa kuyaleta Kigwa umbali wa km 29 kutoka lilipo bomba kuu hadi Kigwa.

Amesema utaratibu utafanywa kwa ajili ya kupeleka maji Kigwa haraka iwezekanavyo na sio kutumia mkandarasi ambaye anaweza kuchukua miaka mitatu.

Kwa mujibu wa baadhi ya wakazi wa eneo hilo, walipoulizwa walisema maji yalijazwa kwenye tanki kwa kupelekwa na gari maalum la maji na baada ya kutumika kwa siku hizo hakikujazwa maji tena.

Chanzo: mwananchi.co.tz