Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi Siha walia kufunguliwa kituo cha afya

Wananchi Siha Izack Laizer Mkazi wa Kijiji mkombozi wilayani Siha mkoani Kilimanjaro

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: Mwananchi

Wananchi wa Kata ya Orkolili wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, wameiomba Serikali kufungua kituo cha Afya kilichopo kwenye kata hiyo ili kuwaepusha kutumia gharama kubwa kufuata huduma hiyo hospitali ya wilaya hiyo.

Wananchi hao wametoa ombi hilo wakati wa ziara ya katibu wa chama cha mapinduzi (CCM),wilayani humo Ally Kidunda kutembelea miradi na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.

Wakizungumza mara baada ya katibu huyo kutembelea kituo hicho cha Afya kilichopo Kijiji cha mkombozi, wameombwa kituo hicho kufunguliwa mapema ili waanze kufurahia kupata huduma karibu na kuepuka kutumia gharama kubwa

"Shukrani ni kitu cha kiungwana Tunamshukuru Rais Samia SuluhuuHassan, Mbunge wetu Godwin Mollel na Diwani wa kata yetu, Jonathan Nasari kwa ujenzi wa kituo hiki karibu tulikuwa tunatumia fedha nyingi kufuata huduma ya Afya hospitali ya wilaya hiyo au kwenda hospitali ya wilaya jirani ya Hai " wamesema wananchi hao

Agnes Aminiel amesema wamekuwa wakiteseka kufuata huduma hiyo Kwenda hospitali ya wilaya hii tunapokuwa na mgonjwa au mjamzito gharama shilingi 15,000 au sh 20000 kwa kutumia badoboda hiyo ni kwenda tu wakati mwingine wakina mama wanajifungulia njia kitu ambacho sio kizuri

"Kwa sasa kituo tunaona ujenzi umekamilika ,tunaomba mkifungue ili kianze kufanya kazi ya kutoa huduma ili kutuepusha kufuata huduma hiyo mbali"amesema Agnes

Pia Izack Laizer Mkazi wa Kijiji cha mkombozi amesema kufunguliwa kwa kituo hicho kwa haraka kitawasaidia hata wazee kupata matibabu wakati mwingine hawana hela na kusabisha kuendelea kuteseka na ugonjwa

"Mimi mwenyewe hapa unaponiona nasumbuliwa na mguu na hapa sina fedha za kuchukua usafiri kwenda hospitali "amesema Laizer

Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Paschal Mbota, amesema kituo hicho kitaanza wakati wowote baadhi ya vifaa vimeshafika bado vitu vidogo vidogo, tunatarajia Septemba mwaka huu huduma ikaanza.

Chanzo: Mwananchi