Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi Rufiji wapata ahueni msaada wa chakula

Nafaka  NAFAKA Wananchi Rufiji wapata ahueni msaada wa chakula

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi wa Kata ya Ngarambe Wilaya ya Rufiji wamepata ahueni baada ya Kaya 803 kupokea magunia 100 ya mahindi, 30 ya mchele pamoja na magunia 11 ya maharage.

Msaada huo wa chakula umetolewa na Kampuni ya Utalii ya Sunset Tarangire leo Februari 16, 2023 na kufanya makabidhiano katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.

Akisoma taarifa fupi wakati wa makabidhiano ya chakula hicho Nurdini Mkumbugo ambaye ni Mratibu wa Maafa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti amesema changamoto ya upungufu wa chakula imesababishwa na mafuriko yaliyotokea Februari, 2022 na kusababisha kuharibu mazao na wananchi kupata mavuno kidogo.

Pia, aliongeza kuwepo wanyama waharibifu wa mazao kutokana na kata hiyo kuwa jirani na Hifadhi ya Selous, pamoja na mvua zilizonyesha chini ya wastani.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji, Maria Katemana ametoa shukrani kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo na kuishukuru Sunset Tarangire kwa kuonesha uzalendo na upendo kwa wananchi na kutoa wito kwa mashirika na taasisi nyingine kutoa misaada kwa wananchi hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live