Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi Moshi wafurika uzinduzi wa safari ya treni

67579 Treni+pic

Sat, 20 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Wananchi wa Moshi mkoani Kilimanjaro na maeneo jirani leo Jumamosi Julai 20, 2019 wamefurika katika viwanja vya stesheni ya Moshi kushuhudia uzinduzi wa safari mpya ya treni ya mizigo.

Hali hiyo inatokana na treni kutoka Dar es Salaam- Tanga hadi Kilimanjaro kusimama kutoa huduma zaidi ya miaka 12 iliyopita.

Uzinduzi huo umefanywa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ambaye ameipokea treni ya mizigo iliyotokea Tanga ikiwa na mabehewa 20.

Miongoni mwa viongozi walioshiriki uzinduzi huo ni msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas, mkuu wa Mkoa wa Tanga,  Martine Shigela ,wakuu wa wilaya ,wabunge pamoja na viongozi  mbalimbali  wa Shirika Reli Tanzania (TRC).

Chanzo: mwananchi.co.tz