Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi Kwimba wapata afueni kufunguliwa kituo matibabu ya macho

WhatsApp Image 2021 07 31 At 11.08.01.jpeg Wananchi Kwimba wapata afueni kufunguliwa kituo matibabu ya macho

Sun, 1 Aug 2021 Chanzo: ippmedia.com

Akizungumza wakati wa tukio hilo lililofanyika leo, Mhandisi Gabriel, ametaka mradi huo uwe endelevu kwani kwa sasa vituo vinavyotoa huduma ya matibabu ya macho mkoani humo vipo 20 kati ya hivyo nane ni vya Serikali na 12 na vya watu binafsi na kwamba kuwepo kwa huduma hiyo jamii kubwa itapata huduma ambayo waliikosa.

Kituo hicho kilichopewa jina la ‘Roshanali Nasser Eye Clinic’ kimejengwa na Dk. Moes Nasser kwa gharama ya Sh. milioni 55 kupitia mradi wa ‘Roshanali Nasser Eye Health Clinic’

"Naagiza uongozi wa Wilaya ya Kwimba kuhakikisha vifaa tiba vinatunzwa na vinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa, Mganga Mkuu wa Mkoa ahakikishe anashughulikia suala la ajira ya moja kwa moja kwa mtaalam alieajiriwa na mradi, kwa huduma za uhakika na wakati wote pamoja na kuhakikisha kumbukumbu sahihi zinahifadhiwa, huduma zinazotolewa na wanaohudumiwa wafahamike isije ikawa tunawatengenezea mwanya wa baadhi ya  watumishi  wachache wasio waaminifu ambapo kihistoria wamekuwepo watu wa aina hiyo," amesema Mhandisi Gabriel

Revocatus Magesa (68), mmoja wa wagonjwa waliopata nafasi ya kupatiwa matibabu ya macho bure wakati wa uzinduzi huo, ameishukuru serikali na wadau wengine kwa kuwasogezea huduma ya matibabu ya macho katika wilaya hiyo.

Amesema kuwa kutokana na umbali mrefu wagonjwa wengine waliamua kubaki na maradhi yao ya macho kwa kushindwa kumudu safari za mara kwa mara kwenda kufuata matibabu.

"Uwepo wa kliniki hiyo wilayani umenirahisishia kupunguza gharama ambapo wananchi wengi walilazimika kusafiri umbali mrefu kutafuta matibabu Jiji la Mwanza," amesema

Meneja Mpango wa Taifa wa Huduma za Macho kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Bernadetha Shilio, amesema katika kila watu 100 watu 20 wanakuwa na matatizo ya macho na kati yao sita wanaupungufu wa kuona unaotibika kwa miwani lakini mtu mmoja utakuta ana ulemavu wa kutokuona kabisa.

"Katika hao watu 20  zaidi ya asilimia 80  ya matatizo yao yanatibika kwa njia rahisi, inawezekana ikawa ni miwani ambayo bei yake ni nafuu au upasuaji ambao unachukua takribani dakika 10 hadi 15 mtu akapona na kuona vizuri na kati ya  mtu mmoja ambaye haoni kabisa asilimia 50 inaletwa na tatizo la mtoto wa jicho.

“Kwa hiyo tujiulize katika mkoa huu ni watu wangapi wasioona kabisa na wangapi wenye tatizo la mtoto wa jicho lakini wakifanyiwa upasuaji ndani ya dakika 10 tu anatoka akiwa anaona na kuendelea na shughuli za uzalishaji mali kwa faida ya familia yake na taifa tukiwekeza katika huduma za macho tutasaidia maendeleo ya nchi" amesema  Shilio.

Naye Meneja wa Mradi wa Roshanali Masser Eye Health Project , Eden Mashayo, amesema jengo hilo lilianza kujengwa mwaka 2013 na limegharimu Shilingi milioni 55 huku vifaa tiba vikiwa vimegharimu zaidi ya Shilingi milioni 115 kwa ufadhili wa Dk.Moes Nasser raia wa Marekani.

Amesema kuwa sambamba na vifaa vya kuanzia, mradi pia nradi huo umeajiri mtaalam mbobezi wa masuala ya macho kwa kipindi cha miezi 18, pia mradi umeshajenga jengo la huduma za macho katika eneo la Nyambiti wilayani Kwimba, ila kutokana na uhaba wa watoa huduma kituo hicho kitakua kikihudumiwa na watumishi kutoka hospitali ya Ngudu

“Sasa tunaiomba serikali isaidie kumuajiri moja kwa moja mtaalam huyu baada ya mkataba wake na sisi, pamoja na kuongeza wataalam wengine,” 

Chanzo: ippmedia.com