Ujenzi wa mradi wa maji Makonde, unaogharimu Sh84 bilioni; umefikia asilimia 40 ya ujenzi wake, huku wananchi wakihimiza ukamilike mapema ili kuondokana na kero ya maji katika maeneo hayo.
Mradi huo ambao umeanza Juni 14, mwaka jana, unatarajia June 30, 2024; ambapo utawanufaisha wakazi wa maeneo ya wilaya za Newala, Tandaimba na Halmashauri ya mji Nanyamba.
Akizungumza na Mwananchi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Makonde Mhandisi Francis Bwire amesema lengo la serikali ni kuona miradi mikubwa na midogo ikikamilika ili kuweza kuondokana changamoto ya upatikanaji wa maji.
“Mfano kwa Tandahimba sasa wana zaidi ya kilomita tatu za mtandao wa mabomba zinatandazwa lakini kuna kilomita 16 zinakuja ndani ya wilaya hiyo, ili kuhakikisha mwananchi anapata maji ndani ya mita 50 kutoka nyumbani kwake na kama mwongozo wa Ewura unavyosema,” anasema Bwire
Sophia Ibrahim mkazi wa Newala amesema kuwa maji yamekuwa ni shida sana hasa ya mvua yanapoisha hivyo kukamilika kwa mradi huu kutaleta neema kwa wakati wa iwlaya za Newala na Tandahimba.
Amesema kuwa wamekuwa wakinunua maji ya kisima kwa Sh200 ambapo ukiwa hauna pesa huwezi kupata maji kukamilika kwa mradi huu kutaleta unafuu wa maisha kwetu.
“Yaani maji tunanunua Sh200 ukiwa hatuna pesa unakaa bila maji majumbani yaani imekuwa ni kero tunaamini kuwa kukamilika kwa mradi huu kwetu ni fursa kubwa hata kiakili tutatulia na kuwaza maendeleo sasa,” amesema Ibrahim.
Godfrey Sijaona mkazi wa Kitangali Newala anasema kuwa anasema kuwa mradi huo utakuwa mkombozi kwakuwa hawana maji.
“Huu mradi ukikamilika maji yatakuwa ni historia mfano hapa kitangali umeme tu ukikata tu masaa machache maji tunaanza kununua maji hadi Sh1500 tunaamini kuwa kukamilika kwa mradi huo ni fursa kubwa kwetu hata umeme nao utaangaliwa” amesema Sijaona
kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanal Patrick Sawala amesema uwa upatikanaji wamaji katika wilaya hiyo ulikuwa ni asilimia 28 ambapo ndani ya miaka miwili imepanda hadi kufikia asilimia 53.
“Tuna zaidi ya miaka upatikanajia wa maji ulikuwa chini ya silimia 28 maji yalikuwa ni changamoto kuwba na katika kipindi cha miaka miwili sasa maji yameboreshwa na miradi ya maji imefanyika na uboreshaji umepanda kutoka aslimia 28 hadi asilimia 53 ya sasa” anasema Kanal Sawala