Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi Kiteto waomba alama za barabarani kuvushia ng’ombe

Mifugo Ya Ngombe 620x308 Wananchi Kiteto waomba alama za barabarani kuvushia ng’ombe

Sun, 27 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kukosekana kwa alama za kupita mifugo barabarani katika baadhi ya maeneo wilayani Kiteto mkoani Manyara, kumesababisha mifugo mingi kugongwa na magari mara kwa mara hivyo wafugaji wengi kufirisika. Wakizungumza kwenye mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto leo Jumapili Agosti 27, 2023 wananchi wamesema maeneo korofi yote wanaombwa yawekwe alama za kuvushia mifugo yao. "Baadhi ya wafugaji Kiteto wamekuwa maskini kwasababu mifugo yao inagongwa na magari ikiwa barabarani... Maeneo korofi ambayo mifugo inagongwa Kiteto ni barabara ya kwenda Tanga, Arusha na Kondoa tunaomba ziwekewe alama,”amesema Mohamed Kinyonga mwananchi wa Kibaya wilayani Kiteto.

Kukosekana kwa alama za kupita mifugo barabarani katika baadhi ya maeneo wilayani Kiteto mkoani Manyara, kumesababisha mifugo mingi kugongwa na magari mara kwa mara hivyo wafugaji wengi kufirisika. Wakizungumza kwenye mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto leo Jumapili Agosti 27, 2023 wananchi wamesema maeneo korofi yote wanaombwa yawekwe alama za kuvushia mifugo yao. "Baadhi ya wafugaji Kiteto wamekuwa maskini kwasababu mifugo yao inagongwa na magari ikiwa barabarani... Maeneo korofi ambayo mifugo inagongwa Kiteto ni barabara ya kwenda Tanga, Arusha na Kondoa tunaomba ziwekewe alama,”amesema Mohamed Kinyonga mwananchi wa Kibaya wilayani Kiteto. Akijibu hoja hiyo Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura) Wilaya ya Kiteto mhandisi Edwine Magiri amesema ni kosa kutembeza mifugo barabarani na kama kuna ulazima basi wafugaji wafuate maeneo maalumu yenye vivuko. "Ni kosa kisheria kutembeza mifugo barabarani na hata ikigongwa taratibu za kisheria huwa zinafuatwa. Wafugaji haswa wa Kiteto waache tabia ya kutembeza mifugo barabarani kwanza ina haribu barabara,"amesema Mhandisi Magiri Kuhusu vivuko amesema katika utaratibu wa kutengeneza barabara huwa kunawekwa vivuko na kama wafugaji wanahitaji maeneo walipo wawasiliane naye ili aendelee kuviweka ili kupunguza adha hiyo kwa wafugaji na wamiliki wa magari pia Mkuu wa wilaya ya Kiteto, Mbaraka Batenga katika mkutano huo amewaeleza wananchi kuwa Serikali itaendelea kupunguza changamoto zinazowakabili zikiwemo elimu, afya, maji na barabara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live