Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi Kigoma wamlilia Rais Samia

Vvv Wananchi Kigoma wamlilia Rais Samia

Sun, 31 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Timu ya Namthamini imetia timu ndani ya mkoa wa Kigoma ikiwa na lengo la kugawa taulo za kike kwa shule mbalimbali za mkoa huo. Katika pitapita za mitaa mbalimbali, tumefanikiwa kuzungumza na wakazi wa Mji huu.

Shabani Omari ambaye ni mvuvi anayemiliki boti ya uvuvi amesema kazi yao inakwenda vizuri isipokuwa baadhi ya changamoto ikiwemo vikwazo vya serikali,"Tunamuomba Rais Samia na serikali yake waangalie upya kuhusu baadhi ya vikwazo wanavyotuwekea kwenye uvuvi. Walikuwa wanatuambia Ziwa Tanganyika lina samaki wengi na hata nusu hatujafikia", amesema Shabani Omari.

"Wenzetu Dar wanaruhusiwa kuvua samaki wote bila kikwazo, hawana utofauti na sisi huku kwetu", ameongeza.

Mkazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Yohana ambaye ni mbeba mizigo katika stesheni ya Kigoma, anasema ameifanya kazi hiyo kwa muda mrefu mpaka sasa lakini changamoto yao ni ufinyu wa safari za treni kuja mkoa huo akiomba kuwepo na safari nyingi kwa wiki.

Kampeni ya Namthamini ipo mkoani Kigoma ambapo inagawa taulo za kike katika shule 6, wilaya ya Kigoma Ujiji na Kasulu. 

#Namthamini #NasimamaNaye 

Chanzo: eatv.tv