Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi Kagera walia na uchafu

Uchafuuuuuuuuu Kg Wananchi Kagera walia na uchafu

Mon, 21 Nov 2022 Chanzo: eatv.tv

Baadhi ya wakazi wa kata za Bilele na Bakoba katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali wananchi ambao wanazalisha taka na kuzitupa katika mto Kanoni, maana kufanya hivyo wanahatarisha afya na usalama wao.

Wakazi hao wamesema kuwa tatizo hilo linasababisha taka kuzagaa hovyo na kwamba asilimia kubwa ya wanaofanya vitendo hivyo wanafanya makusudi, maana ni maeneo machache ambayo hayana sehemu za kukusanyia taka

Wakizungumzia tatizo hilo wenyeviti wa mitaa ya Buyekera Asili na Mtoni wamewataka wananchi kuacha tabia hiyo mara moja na badala yake watumie maeneo yaliyoandaliwa kwa ajili ya kutupa taka, huku diwani wa kata Bakoba, Shaban Rashid akidai wakaobainika kuendelea na vitendo hivyo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za halmashauri  

Chanzo: eatv.tv