Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi Geita walalamikia mgodi wa GGML uharibifu vyanzo vya maji

GGM GEITA (600 X 929) Wananchi Geita walalamikia mgodi wa GGML uharibifu vyanzo vya maji

Mon, 15 Nov 2021 Chanzo: Wananchi Geita walalamikia mgodi wa GGML uharibifu vyanzo vya maji

Wananchi wanaoishi karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) katika Mtaa wa Nyamalembo eneo maarufu la Mizingamo Mjini Geita wamelalamika kutumia maji machafu ya Bwawa la Nyankanga lililopo katika eneo hilo, hali ambayo imezidi kuhatarisha usalama wa afya zao.

Wananchi hao wamedai kwamba kwa muda mrefu wamezuiwa kuendeleza maeneo yao baada ya kuwa ndani ya leseni ya Mgodi huo jambo ambalo limesababisha kutokupelekewa huduma muhimu za kijamii ikiwemo maji safi na salama.

"Tunapikia, tunaoga, tunayategemea haya maji, tunaharisha hadi damu, tunatoka upele kuna muda mlipuko unatokea tunaumwa kijiji kizima,

"Tunawaomba hata watupe tu fidia, Serikali iingilie kati, hatuna namna ya kupata huduma za kijamii, tumeomba kuhamishwa ila GGM amegoma amesema ana utaratibu wake, tunateseka" amesema mwananchi huyo.

Uongozi wa Mgodi wa GGML kupitia kwa Meneja wa Mashauriano, Mashirikiano na Mashirika mengine Manace Ndoroma amezungumzia sakata hilo na kusema kwamba kama majirani ni vyema wakaishi kwa kuheshimiana.

“Tuna sisitiza kwamba kama majirani tukaishi kwa kuheshimiana na kila mmoja kumsaidia mwenzake kulinda mali yake, sisi haki ardhi hatutaigusa bila kufuata sheria lakini na wewe haki madini si yako na hujapata kibali cha kuichimba basi mwachie Amesema Meneja huyo.

Nae, Diwani wa kata hiyo Prudence Temba, amesema kuwa anatamani kuishauri Serikali iweze kutatua sakata hilo kwani wanaoathirika zaidi ni wanakijiji hao.

Chanzo: Wananchi Geita walalamikia mgodi wa GGML uharibifu vyanzo vya maji