Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi Dar kupimwa magonjwa ya moyo

Sindano Vifoooo Wananchi Dar kupimwa magonjwa ya moyo

Fri, 18 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Hospitali ya Dar Group wanatarajia kufanya kambi maalum ya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Anna Nkinda imesema upimaji huo utafanyika kwa watoto na watu wazima kuanzia Septemba 02, 2023 hadi Septemba 03,2023 kuanznia saa mbili asubuhi hadi saa 10 alasiri jioni katika Hospitali ya Dar group iliyopo Temeke .

“Aidha katika kambi hii kutakuwa na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora, ambayo itawapa wananchi uelewa na kufuata mtindo bora wa maisha na kuepukana na magonjwa yasiyoambukizwa yakiwemo ya moyo, ambayo yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu,”ameeleza Nkinda.

Amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao kujua kama wana matatizo ya moyo, ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa na magonjwa na kusisitiza kuwa huduma hiyo itakuwa ya kuchangia gharama ya matibabu.

“Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0754578190 ya Dk Tulizo Shemu,0684345921, Flaviana Masegesa na 0674179036 ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live