Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi 49 kulipwa fidia ya Sh3.9 bilioni

Fedha Ed Wananchi 49 kulipwa fidia ya Sh3.9 bilioni

Wed, 11 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kuwa serikali italipa kiasi cha Sh bilioni 3.9 kwa wananchi 49 ikiwa ni fidia ya awamu ya pili yakupisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma mkoani Mara.

Bashungwa amesema kuwa tayari kiasi hicho kimewasilishwa Wizarani ili kuendelea kulipa wananchi hao waliobakia. Tayari wananchi 85 walilipwa zaidi ya Sh bilioni 4 katika awamu ya kwanza.

Bashungwa amempongeza Mbunge wa Musoma Mjini, Vedasto Mathayo kwa kuendelea kufuatilia kwa karibu mradi wa ujenzi wa Kiwanja hicho pamoja na fidia kwa wananchi hao.

“Mheshimiwa Mbunge Vedasto umekuwa mkali sana juu ya fidia kwa wananchi wako na Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan tayari amesikia kilio chako, tutaendelea kushirikiana kuhakikisha tunamaliza suala hili angalau kwa awamu ili tulikamilishe", amesema Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amesema kuwa Serikali itahakikisha inalipa madeni ya Mkandarasi kwa wakati ili kuwaweza kuendelea na kazi kwa kuongeza kasi ya ujenzi na kukamilisha kwa viwango bora kama ilivyo kwenye mkataba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live