Wananchi zaidi ya Elfu kumi katika Tarafa ya Endabash wilayani Karatu Mkoani Arusha wameondokana na adha ya maji waliokuwa wakikabiliana nayo baada ya Shirika la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na serikali kufanikisha ujenzi wa Miradi minne ya maji.
Miradi hiyo ambayo imehusisha ujenzi wa Visima vya maji Ulazaji wa Mabomba, ujenzi wa Matanki, uwekaji wa Vituo vya Maji, na Mitambo ya Umeme wa Jua, inatajwa kugharimu takriban milion mia nane
Miongoni mwa Wananchi wanaonufaika na miradi hiyo ni kutoka vijiji vya Gidibaso pamoja na Endamararieki na hapa ni baadhi ya wananchi wakielezea furaha yao
Ester Mshendwa ni Kaimu Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Kaskazini anaeleza Matamanio yao kuwa ni kuona Miradi hiyo inakuwa Endelevu kwa kusimamiwa na serikali,huku Mkuu wa Wilaya ya Karatu akiahidi serikali kusimamia vyema miradi hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Karatu Dadi Kolimba amesema ametoa hakikisho la Kutunzwa kwa miradi hiyo kwa manufaa ya vizazi wa sasa na Vijavyo
Mbali na Miradi ya Maji, World Vision Tanzania kwa Wilaya ya Karatu inajihusisha pia na miradi ya Elimu na Afya hasa kwa watoto katika tarafa za Endabashi na Lake Eyasi.