Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanakijiji wahoji kukosa umeme katikati ya bomba la gesi

75778 Wanakijiji+pic

Mon, 16 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakazi wa kijiji cha Mangwi wilayani Kibiti mkoani Pwani wamehoji sababu za kukosa umeme wakati eneo hilo limepita bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.

Kijiji hicho chenye vitongoji vinne vyenye wakazi  takribani 360 ni miongoni mwa vijiji vilivyopitiwa na mradi wa bomba hilo la gesi.

Kwa mujibu wa Shirika la Taifa la Maendeleo ya Petroli (TPDC), bomba hilo linasafirisha makadirio ya gesi asilia futi za ujazo milioni 90 kwa siku kutoka kituo cha kuchakata gesi Madimba, Mtwara.

Zaidi ya asilimia 55 ya umeme wa gridi ya Taifa kwa sasa unategemea uzalishaji wa gesi hiyo.

Katika kutambua mchango wa wanakijiji waliopitiwa na bomba hilo, leo Jumamosi Septemba 14, 2019, TPDC imetoa msaada wa vifaa katika kituo cha afya kijijini hapo ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano yake na jamii.

Hata hivyo, wakati wa mapokezi ya msaada huo, wananchi hao wamehoji kijiji hicho kukosa umeme wa gesi.

Pia Soma

Advertisement

Viongozi wa CCM akiwamo wenyekiti wa chama hicho kata ya Mchukwi, John Nagga wameeleza jambo hilo na kudai kuwa jambo hilo limekuwa kero na huenda likawa tishio katika uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019.

Mohamed Mpwawa, mkazi wa kijiji hicho amesema kukosekana kwa umeme kunakwamisha shughuli za uchumi.

"Yaani tunajiuliza tunakosa majibu iweje bomba lipite, nyaya zipite hadi kata ya mbele lakini sisi hatuna umeme, hii si sawa kabisa tunaomba Serikali itazame suala hili,” amesema Mpwawa.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewatoa hofu wakazi wa kijiji hicho, akisema Serikali imeagiza uhakiki wa vitongoji vyote nchini ambavyo havikupata huduma ya umeme kupita mradi wa Rea.

Mgalu amesema Serikali kwa kujali wananchi maeneo ya vijiji imeendelea na utekelezaji wa mradi wa Rea na awamu ijayo, baadhi ya vijiji vitaanza kuunganishwa wilayani Kibiti.

Kuhusu msaada huo ,Mkurugenzi wa TPDC, Dk James Mataragio amesema msaada huo ni sehemu ya mchango wa shirika hilo katika vijiji vilivyopo katika miradi yake.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz