Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanakijiji wafurahia muuza bangi kukamatwa

Bangi Pic Wanakijiji wafurahia muuza bangi kukamatwa

Fri, 10 Feb 2023 Chanzo: Mwananchi

Wananchi wa Kijiji cha Sanya Hoyee Wilayani Siha, Mkoa wa Kilimanjaro, wamepongeza viongozi wa kijiji hicho kwa kufanikiwa kukamatwa mwanamke mmoja anayefanya biashara haramu ya kuuza bangi kwenye kijiji hicho na kisha kufishwa Kituo cha Polisi Sanya Juu.

Wananchi hao wakiongea na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti, wamesema kitendo cha kukamatwa mwanamke huyo ni kimewafurahisha kwani bangi imekuwa ikivutwa hovyo mitaani na vijana na kuonekana ni jambo la kawaida.

"Ni kweli tunawapongeza viongozi wetu kwa kuanza kushirikiana na Polisi kukamata wanaouza dawa za kulevya ili vijana wetu wawe salama,"alisema mmoja wa wananchi hao ambaye hakutaka jina lake kutajwa.

Amesema mwanamke kwa muda mrefu eneo la mabanzini amekuwa akionekana akifanya biashara ya kuuza vinywaji mbalimbali lakini kumbe anayo nyingine haramu ya kuuza madawa ya kulevya kitendo ambacho siyo kizuri.

Yakobo Zakaria amesema uvutaji wa bangi limekuwa jambo la kawaida, unakuta mtoto mdongo anavuta bangi bila aibu, unajiuliza ameitoa wapi. Wakati mwingine ukimuuliza anakuwa mkali anakutishia usimfuatilie maisha yake atakudhuru.

Niwapongeze kwa jitihada hizi za kupiga vita dawa hizo, kwani vijana wanaharibika kwa kuvuta dawa hizo na kuanza kuwa wezi wa vitu mbalimba na kusababisha maendeleo kurudi nyuma jamii.

Aisha Juma ametaka ushirikiano wa pamoja kupiga vita dawa hizo anapokamatwa mtu apelekwe kwenye vyombo husika na kupewa adhabu na siyo anakamatwa siku mbili anaonekana mtaani akiendelea na biashara zake.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Moses Munuo amekiri kukamatwa kwa mwanamke huyo na kuomba ushirikiano kutokomeza dawa hizo ili kizazi kibaki salama na chenye maadili.

Chanzo: Mwananchi