Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanahabari wapewa msaada kujikinga na corona

MSANDO.jpeg Wanahabari wapewa msaada kujikinga na corona

Tue, 28 Apr 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAKILI wa kujitegemea, Alberto Msando, ametoa msaada wa barakoa 100 na vitakasa mikono 100, kwa waandishi wa habari Mkoa wa Arusha ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Akikabidhi msaada huo, leo Aprili 28,2020 kwenye Ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC), Msando amesema wanahabari ni watu muhimu wanaoandika habari za ugonjwa wa corona hivyo wanatakiwa kupewa vifaa vya kujikinga na ugonjwa huo.

Amesema waandishi wa wanatakiwa kutoa taarifa sahihi na kutoa elimu ya namna ya kudhibiti ugonjwa huo katika jamii.

“Waandishi wa habari toeni elimu kwa jamii kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa corona ikiwemo kuwaambia wananchi kuchukuwa tahadhari zinazotolewa na wataalamu wa afya ili kujikinga na ugonjwa huo.

Hata hivyo, amesema waandishi wa habari wana mchango mkubwa katika utoaji wa taarifa, hivyo katika kipindi hiki cha maambukizi ya corona amewataka kufanya kazi za kiuchumi zitakazowaingizia sambamba na kuchukuwa tahadhari.

"Lazima mchukue tahadhari ya ugonjwa huu wa corona kwa kuandika habari sahihi na habari hizo wananchi lazima wazijue ,"amesema Msando.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandisi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC), Claud Gwandu, ameshukuru kwa msaada huo, na amesema utakuwa msaada kwa waandishi wa habari kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

Licha ya kuzungumza hayo, ametoa rai kwa wadau wengine kujitoa kuwasaidia wanahabari katika hatua ya kupambana na ugonjwa wa corona.

Wakizungumza kwa niaba ya waandishi wa habari Mkoa wa Arusha, Lillian Joel,Cynthia Mwilolezi na Hababi Mohamed,wameshukuru kwa msaada huo, na kusema utawasaidia kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live