Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanahabari Mbeya wampongeza Dk. Mpango

75799 Pic+mpango Wanahabari Mbeya wampongeza Dk. Mpango

Wed, 31 Mar 2021 Chanzo: ippmedia.com

Akizungumza na Nipashe, makamu mwenyekiti wa chama hicho, Joseph Mwaisango, amesema wanaamini kuwa uhuru wa vyombo vya habari utakuwa mkubwa, watapata ushirikiano kwenye vyanzo mbalimbali vya habari ili kutimiza jukumu lao la kuhabarisha watanzania.

Amessema anaamini Serikali itaendeleza mazuri yaliyoasisiwa na Hayati Dk. Magufuli katika kuisadia tasnia ya habari kusonga mbele ikiwemo kuanzishwa kwa sheria mpya ya huduma ya vyombo vya habari ambayo imelenga kuboresha sekta hiyo.

"Tunaungana na Watanzania wote kumpongeza Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, pamoja na Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango, kukubali kuwatumikia Watanzania, tunatamani kufanya kazi kwa uhuru na kupewa ushirikiano pale tunapohitaji taarifa mbalimbali," amesema.

"Nia yetu ni kulisaidia taifa kusonga mbele, tumeshuhudia baadhi ya vyombo vya habari vikichukuliwa hatua mbalimbali ikiwamo kufungiwa au kulipa faini kutokana na sababu mbalimbali najua kwa utawala huu busara na sheria vitatawala zaidi ili kuijenga Tanzania," amesema Mwaisango.

Katika hatua nyingine, Mwaisango ameiomba serikali kuendelea kutumia vyama vya Waandishi wa Habari kutoa elimu juu ya masuala mbalimbali kwa sababu wao ni daraja la kufikisha ujumbe kwa wananchi.

Chanzo: ippmedia.com