Jumla ya wanafunzi 1,648 wa kidato cha Pili na cha Nne waliopo wilayani Newala mkoani Mtwara wameacha shule kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo Mimba, hamahama ya wazazi kwa ajili ya kilimo, hali ngumu ya maisha, wazazi kutengana na wao wenyewe kutokuwa na mwamko wa elimu.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira wa wilaya hiyo Mwl. Bashiru Malocho alipokuwa anazungumza na Mashujaa Fm ambapo ameeleza kuwa wanafunzi 881 ni kutoka kidato cha Pili na wanafunzi 767 ni kidato cha Nne
Aidha amesema kati ya wanafunzi hao 1,031 ni kutoka halmashauri ya wilaya ya Newala (Newala vijijini) huku 617 wakitokea halmashauri ya mji Newala
Hata hivyo Mwl. Malocho amewaasa wazazi wilayani humo kuwekeza kwa watoto wao kielimu ili iwanufaishe baadae kwani serikali imeendelea kuondoa kero ambazo hupelelea watoto kuacha shule ikiwemo ujenzi wa madarasa na michango isiyo na tija