Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi wenye ulemavu watoa ya moyoni

141e3b2a9b7d0f80af4bb6402133016b.jpeg Wanafunzi wenye ulemavu watoa ya moyoni

Tue, 24 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WANAFUNZI wenye ulemavu wanaosoma shule za msingi mkoani hapa wameiomba serikali inapotoa nafasi ya ajira kwenye kanda mbalimbali ikiwemo ya walimu, itoe upendeleo kwa kuajiri walimu wa elimu maalumu ili kukabiliana na upungufu uliopo mashuleni.

Ushauri huo ulitolewa na Katibu Msaidizi wa Baraza la Watoto Wenye Ulemavu, Janeth Silyvester alipozungunza kwenye mafunzo ya asasi za kiraia kuhusu ushawishi na utetezi wa watu wenye ulemavu iliyofanyika mkoani hapa.

Silyvester ambaye ni mwanafunzi wa shule ya viziwi Dodoma alisema kuna upungufu mkubwa wa walimu hao wenye sifa maalumu ya kufundisha watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali wakiwemo na wasiosikia.

Alisema kukosekana kwa walimu wenye sifa kwenye shule hizo zenye mahitaji maalumu imesababisha wakose walimu wanaoweza kuwafundisha kwa kutumia sifa waliyonayo.

Hata hivyo wanafunzi hao wameiomba serikali kuhakikisha walimu waliopo wenye sifa hiyo maalumu wahakikishe wanapelekwa kwenye shule zenye mahitaji maalumu kutokana na makundi ya watu wenye ulemavu badala ya kuendelea kufundisha katika shule ambazo hazina changamoto zinazohusu ulemavu.

Chanzo: habarileo.co.tz