Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi wawili wafa maji wakiogelea

9342 Pic+wanafunzi TZW

Sat, 16 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Wanafunzi wawili wa darasa la kwanza wa Shule ya Msingi Kasomeko katika Kijiji cha Kasomeko wilayani Sengerema mkoani hapa, wamefariki dunia wakati wakiogelea kwenye dimbwi la maji karibu na nyumbani kwao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Juni 13 saa kumi na moja jioni.

Aliwataja watoto hao kuwa ni Shija Kamlete (8) na Baraka Kapalale (8).

Kamanda Msangi alisema dimbwi hilo lilitokea baada ya kuchimbwa vifusi vya mchanga vilivyosambazwa barabarani.

Alisema watoto wa kijiji hicho walikuwa na tabia ya kwenda kuogelea kwenye dimbwi hilo hivyo hata hao waliingia kuogelea lakini maji yaliwazidi nguvu na kushindwa kutoka ndipo wakazama.

Wakati huohuo; Watu tisa wakiwamo waganga wa jadi wilayani Misungwi, wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kushiriki mauaji ya mkazi wa Kijiji cha Lubili, Manungwa Nkwabi (20) aliyenyongwa kwa khanga na watu wasiojulikana.

Kamanda Msangi alisema kwamba tukio hilo lilitokea Juni 13 wakati Manungwa alipokuwa akitoka kuchanja kuni porini akiwa ameongozana na mwenzake wa kike ambaye hakutajwa jina na kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha mauaji hayo yametokana na imani za kishirikina.

Alisema wasichana hao, walipofika eneo la tukio walikutana na kijana mmoja ambaye alimvuta na kuanza kumnyonga Manungwa huku mwenzake akikimbia kuomba msaada kwa wananchi lakini walipofika walikuta tayari amefariki dunia na mtuhumiwa kutokomea kusikojulikana.

Alisema wakati upelelezi ukiendela tayari mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko.

Chanzo: mwananchi.co.tz