Kaimu kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoani Kigoma, Jacob Chacha amesema kupata miili ya watoto wawili kati ya nne waliozama mto Luiche Kigoma jana Ijumaa, Februari 24, 2023 majira ya saa 2 asubuhi wakiwa wanavuka na mtumbwi kuelekea shule ya msingi Kagera.
Katika ajari hiyo wanafunzi waliokuwa wanavuka walikuwa 6 ila wawili waliweza kuokolewa wakiwa hai na wanne kupotelea mtoni, hivyo leo Februari 25, jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeweza kupata miili ya wanafunzi wawili ambao ni Zabibu Jumanne na Ramadhani matatizo.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wanaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Kigoma kuwatafuta miili ya watoto wengine wawili hambao bado haijapatikana.