Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi wawataka madereva kuwa makini

57195 Pic+usalama

Tue, 14 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge ambao ni mabalozi wa usalama barabarani wametoa kilio chao wakiwataka madereva wa vyombo vya moto kuongeza umakini wanapokuwa maeneo ya shule ili kupunguza uwezekano wa kutokea ajali zinazogharimu maisha ya watoto wengi.

Mabalozi hao ambao wapo chini ya kampuni ya mafuta ya Puma Energy wameeleza kuwa vifo vingi vya watoto vinatokana na ajali hivyo ni jukumu la jamii kupaza sauti kukabiliana na hali hiyo.

Kulingana na ripoti ya Global Status, ajali za barabarani zinaongoza kusababisha vifo vya watoto na vijana kuanzia miaka 5 hadi 29.

Wakizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa ya nenda kwa usalama, wanafunzi hao walisema ni muhimu kwa madereva kuzingatia sheria na alama za barabarani ili kupunguza uwezekano wa kutokea ajali.

“Ni muhimu kwa madereva kuzingatia sheria za barabarani, kuongeza umakini na kuchukua tahadhari wanapokuwa maeneo ya shule au kwenye makazi ya watu kwa kuwa mara nyingi watoto wanacheza bila kujua hatari iliyopo mbele yao, wakiwahurumia wataokoa maisha yao,” amesema Nelian Edwin mwanafunzi wa darasa la sita.

Naye Godbless Mlacha alisisitiza watoto kupewa elimu ya usalama barabarani ili wachukue tahadhari wanapokuwa katika maeneo hatarishi na yenye magari mengi kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika.

Pia Soma

Katika maadhimisho hayo ambayo mwaka huu yalibebwa na kauli mbiu ‘Sema usikike, okoa maisha’ wanafunzi hao walikwenda kwenye kituo cha mafuta cha Puma Seaview na kuzungumza na madereva waliofika katika kituo hicho.

Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah alisema kampuni hiyo imeamua kujitosa kwenye kampeni ya usalama barabarani baada ya kuona watoto ni waathirika wakubwa.

“Ukiangalia takwimu kundi kubwa la wanaopoteza maisha kutokana na ajali za barabarani ni watoto na sisi tukaona ipo haja kuwatumia watoto hawa kutoa elimu kwa umma ili watu waelewe ni nguvu kazi gani inapotea, na ndiyo sababu tunahamasisha kila mmoja awe sehemu ya kupaza sauti,” alisema Dhanah.

Chanzo: mwananchi.co.tz