Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi wasomea chini tangu 1942

Kongwe shule ya mwaka 1942

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: ippmedia.com

JUMLA ya wanafunzi 214 kati ya 662 wa Shule ya Msingi Bugunda, iliyopo Kata ya Bwasi, jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, wanasomea chini ya miti kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.

Shule hiyo ina vyumba sita vya madarasa, mahitaji halisi ni vyumba 14, hali inayochangia mrundikano wa wanafunzi madarasani hadi wengine kusomea nje na pia walimu wanaohitajika ni 15 lakini waliopo ni saba tu.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Alexander Materu, alisema, tayari serikali kupitia mradi wake wa EP4R imetoa Sh. milioni 40 ili kukamilisha ujenzi wa madarasa mawili, ofisi moja ya walimu na ununuzi wa madawati.

"Shule ilianzishwa mwaka 1942, ina wanafunzi 662 ilam ina changamoto nyingi, lakini zinaendelea kutatuliwa na wadau mbalimbali wa elimu ili kusaidia watoto kusomea katika mazingira mazuri," alisema Materu.

Mtendaji wa Kijiji cha Bugunda, Mashaka Kagere alisema, wakazi wa kijiji hicho wanachangia michango kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule yao ikiwa ni pamoja na kuchimba msingi wa madarasa mawili na ofisi ya walimu.

Alisema, wakazi wa Bugunda pia wanaasomba mawe, mchanga na maji kwa ajili ya ujenzi huku wadau wengine wa elimu wakichangia ujenzi wa matundu nane ya choo cha wanafunzi.

"Shirika lisilo la kiserikali la Project Concern Internation (PCI) limejenga matundu nane ya choo cha wanafunzi, mbunge Prof. Sospeter ametoa madawati 46, vitabu zaidi ya 1,000, Mfuko wa Jimbo umechangia madawati 54, halmashauri yetu ilishachangia Sh. milioni tano," alisema Kagere.

Aidha, mtendaji huyo wa kijiji, aliwaomba wadau wengine wa elimu wakiwamo wazaliwa wa Bugunda kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu kwenye shule hiyo kongwe.

Chanzo: ippmedia.com