Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi wasiolipia chakula wadaiwa kufungiwa darasani

Kiongozi Mbio Za Mwenge Afunguka Ongezeko La Vyumba Vya Madarasa Wanafunzi wasiolipia chakula wadaiwa kufungiwa darasani

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga, ambao wazazi wao wameshindwa kulipia chakula na mitihani ya kila mwezi, wanadaiwa kufungiwa darasani ili wasirejee nyumbani kwao kula.

Utaratibu huo unadaiwa upo kwa muda mrefu na wazazi wanapohoji, huambiwa wahamishie watoto wao katika shule zisizokuwa na michango ya aina yoyote.

Hayo yamebainishwa juzi na baadhi ya wazazi na walezi katika mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika sekta ya afya, elimu, maji, kilimo, ardhi na miundombinu ya barabara uliofanyika katika Kata ya Majengo.

Mmoja wa wazazi, Ruben Macheyeki amesema, wanafunzi wa darasa la kwanza, pili, tatu, tano na sita wanatakiwa kutoa Sh. 5,000 ya uji kila mwezi huku wanafunzi wa madarasa yenye mitihani ya darasa la nne na saba wanatozwa Sh. 3,000 ya mitihani ya mwezi na Sh. 3,500 ya chakula cha wiki.

“Siku za mitihani kwa wanafunzi ambao hawajatoa fedha za mitihani huchapwa bakora na kuwaaguza watuambie tuwahamishie shule ambazo hazina michango, suala hili limekuwa likituchonganisha na watoto wetu wakituona hatuwajali kabisa," amesema Macheyeki.

Salome William amesema wanafunzi wa sekondari kila mmoja anachangishwa kilo 15 za mchele, saba na nusu za maharage na Sh.10,000 kwa ajili ya malipo ya mpishi pamoja na ununuzi wa kuni za kupikia.

Ameiomba serikali iingilie kati ili watambue uhalali wa michango hiyo kwa wote wanahitaji watoto wao wasome.

Akijibu malalamiko hayo, Ofisa Elimu Msingi Hamida Kaganda amesema, suala la chakula shuleni ni lazima na linapangwa baina ya wazazi na bodi za shule kwa viwango vinavyotakiwa kutolewa.

Aidha, amesema hana taarifa ya michango mingine na kuahidi kufuatilia na kuchukua hatua kwa wanaofanya hivyo.

Ofisa Elimu Sekondari, Anastazia Manumbu amesema, alifuatilia malalamiko hayo na kubaini Sekondari ya Kishimba ndio inayochangisha michango ya fedha za mitihani ya kila mwezi kwa madarasa yenye mitihani.

Ameahidi kukutana na wakuu wa shule na wazazi kujadili na kutatua kwa pamoja changamoto hiyo.

Mkuu wa Mkoa huo, Christina Mndeme, amewaagiza maofisa elimu wa shule za msingi na sekondari, walimu wakuu, wazazi pamoja na maofisa elimu kata kukaa kwa pamoja na kutatua malalamiko hayo, kwani serikali imepiga marufuku michango isiyokuwa na tija kwani inaumiza mzazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live