Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi wasahau kusoma baada ya Covid 19

3796ef6e7beb23429d805114c2a77b19 Wanafunzi wasahau kusoma baada ya Covid 19

Thu, 30 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KUTOKANA na likizo ya ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu unaosababishwa na virusi vya corona, baadhi ya wanafunzi wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro wamerejea shuleni wakiwa wamesahau kusoma, kuandika na kuhesabu.

Mfumo uliokua umewekwa na serikali kipindi ambacho wanafunzi hawaendi shule ilikua ni kusoma kupitia vituo vya redio na televisheni.

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kyoo na Maua za Wilayani Moshi, Kilimanjaro, Kepha Masamu alisema hali hiyo imetokana na wazazi kutumikisha wanafunzi wakashindwa kujisomea

"Wanafunzi walitumikishwa hata mwishoni mwa wiki au sikukuu hawataki kukaa nyumbani wanaomba waje shule kuepuka kutumikishwa," alisema.

Serikali ilizifunga shule zote nchini Machi 17, kutokana na mlipuko wa virusi vya corona ambao takwimu zinaonesha jumla ya watu 509 waliambukizwa nchini huku vifo vikiwa 21.

Katika takwimu za Shirika la Afya Dunia (WHO) mpaka sasa zaidi ya watu milioni 14 wameambukizwa virusi vya corona huku vifo vikiwa zaidi ya milioni sita duniani kote.

Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), wanafunzi 250,000 ulimwenguni imetatizwa kutokana na janga la virusi vya corona linaloendelea kuitikisa dunia, ambapo mataifa 120 yalifunga shule zake ili kudhibiti maambukizi hayo.

Baadhi ya wanafunzi walieleza kutumikishwa kwa kuuza bidhaa sokoni badala ya kuwaacha nyumbani kujisomea kipindi ambacho shule zimefungwa kwa sababu ya virusi vya corona.

Mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Maua, Baraka Emmanuel alisema "Sikupata muda kujisomea, nilimsaidia babu kuuza duka".

Mwanafunzi wa darasa la nne, Upendo Joseph alisema "Nilikua nafanya kazi za nyumbani, namsaidia dada amejifungua, hivyo nilikua nampikia na kumwekea maji ya kuoga, kufua na kazi nyingine, sikupata muda wa kusoma".

Benadertha John anayesoma darasa la saba alisema "nilikua naenda sokoni kumsaidia mama kuuza vitu, sikujua kama kuna vipindi redioni na televisheni, sikufuatilia"

Mzazi wa Blanka Joseph alisema: "Nimesikitika shule kufunguliwa, watoto walinisaidia kazi za nyumbani, sasa hivi namenyeka mwenyewe".

Chanzo: habarileo.co.tz