Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi waliokufa kwa kukanyagana waagwa

94894 Pic+kenya Wanafunzi waliokufa kwa kukanyagana waagwa

Sun, 9 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kakamega. Familia zimeungana na waombolezaji wengine kuwaaga wanafunzi 14 waliokufa kwa kukanyagana katika Shule ya Msingi Kakamega nchini Kenya.

Katika ibada ya kuaga miili hiyo, majeneza yenye miili ya watoto hao ilipangwa na wanafunzi wa shule hiyo wakakaa pembeni mwake. ]

Viongozi mbalimbali wa kisiasa na dini pamoja na wafanyakazi wa chama cha msalaba mwekundu walikusanyika katika shughuli iliyotawaliwa na masikitiko.

Matokeo ya uchunguzi

Mapema, matokeo ya uchunguzi wa miili hiyo yalionyesha kwamba wanafunzi sita kati ya 14 waliofariki katika mkanyagano walifariki baada ya kukosa hewa.

Daktari anayehusika na uchunguzi wa miili hiyo, Dickson Mchana amesema kundi la maafisa bado linaendelea na uchunguzi kuhusu sababu za vifo vya wanafunzi wengine wanane.

Pia Soma

Advertisement
‘’Tunaharakisha uchunguzi ili kutoa matokeo kwa lengo la kuandaa miili ili ichukuliwe na familia kwa ibada ya mazishi itakayofanyika katika uwanja wa Bukhungu mjini Kakamega’’, alisema Dk Mchana.

Maafisa wa polisi bado wanachunguza kisa hicho  kilichosababisha wanafunzi 39 wakijeruhiwa.

Wamechukua maelezo ya walimu, wanafunzi na mashahidi ili kubaini kilichosababisha mkasa huo.

Wanafunzi wawili wanapata matibabu katika hospitali kuu ya Kakamega.

Chanzo: mwananchi.co.tz