Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi walioiba viti Shule ya Sinoni walipa mil 5.4/-

01adcda6bac50a267c6d2b81bd150de4 Wanafunzi walioiba viti Shule ya Sinoni walipa mil 5.4/-

Sat, 19 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Wazazi na wanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Sinoni walioiba viti 108 na walionunua viti hivyo leo (Ijumaa, Desemba 18, 2020) wamelipa Sh milioni 5.4 kwa ajili ya utengenezaji wa viti vingine.

Malipo hayo yamefanyika ili kutekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini, Kenani Kihongosi aliyeagiza ulipwaji wa fedha hizo ili kununua viti vingine baada ya kukamatwa kwa wanafunzi hao pamoja na waliovinunua.

Sakata hilo la wizi wa viti shuleni, lilimlazimu Mkuu wa Wilaya kuwacharaza viboko wanafunzi hao pamoja na wafanyabiashara walionunua vitu vilivyokuwa vimenunuliwa kutoka kwa wanafunzi hao.

Chanzo: habarileo.co.tz