Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi, walimu wajisaidia vichakani kwa miaka mitatu sasa

Kujisaidia Mwandamizi Wanafunzi, walimu wajisaidia vichakani kwa miaka mitatu sasa

Mon, 8 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya wazazi wa wanafunzi wanaosoma Shule ya Msingi Tembo Mashujaa, mjini Songea wametishia kutorejesha shuleni watoto wao kutokana na choo cha wanafunzi shuleni hapo kujaa.

Waandishi wa habari hizi wameshuhudia kujaa kwa choo hicho chenye matundu 10, ambacho kinatumiwa na wanafunzi takribani 800.

Wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo wameuomba uongozi wa wilaya kunusuru watoto wao dhidi ya hatari ya choo hicho kujaa na kuweka rehani afya na maisha ya wanafunzi na walimu.

UONGOZI WA SHULE

Mwenyekiti wa Kamati ya Shule hiyo, Masumbuko Mbogoro, amesema mazingira ya choo ni mabaya kwa sababu matundu yote 10 yameziba na kusababisha haja kubwa kuzagaa.

Ameomba uongozi wa manispaa kuchukua hatua za haraka, kusaidia ujenzi huo kwa kuwa mvua inayoendelea kunyesha itasababisha mlipuko wa magonjwa hasa ya kuambukiza, kama vile kipindupindu.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tembo Mashujaa, Mary Mpyambala, amethibitisha tatizo lipo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.

Amesema shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 800 ambao wengi wao wakibanwa haja, hulazimika kwenda kujisaidia porini, hivyo kuwa hatarini kupata magonjwa ya kuambukiza na kung'atwa na wadudu kama nyoka na hata kushambuliwa na wanyama wakali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live