Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi walazimika kukimbia shule kisa unyanyasaji wa kingono

Mgomo Spiring Valeny Wanafunzi walazimika kukimbia shule kisa unyanyasaji wa kingono

Mon, 14 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanafunzi 25 wanaosoma kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Spring Valley Mkoani Iringa wanadaiwa kuondoka Shuleni hapo na kugoma kurudi kutokana na wenzao wanne kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji wa kingono vinavyodaiwa kufanywa na Meneja wa Shule hiyo.

Inadaiwa siku ya jumamosi waliandamana kwenda katika kituo cha polisi kutoa taarifa na baadaye dawati la jinsia kulazimika kuwapeleka katika Sekondari ya Lugalo iliyopo Manispa ya Iringa.

Mwalimu wa Malezi Lugalo Hawa Kibona amethibitisha kupelekwa kwa Watoto hao jumamosi jioni ya saa12 na kupewa hifadhi.

Akiongea kwa njia ya simu Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya iringa Tiniel Mbaga amesema Watoto hao wamekuwa wakipokea vitisho vya kufukuzwa Shule kutoka kwa Meneja na hivyo wakaamua kuondoka Shuleni hapo.

Meneja wa Shule pamoja na Mkuu wa Shule wamechukuliwa na Polisi huku Wanafunzi hao wakiendelea kuwepo Sekondari ya Lugalo na mustakabali wao utajulikana leo Jumatatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live