Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi wakosa masomo kisa choo

41892 VYOO+PIC Wanafunzi wakosa masomo kisa choo

Sat, 16 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Zaidi ya wanafunzi 750 wa shule ya msingi Morotonga wilayani hapa  hawasomi kufuatia idara ya afya kuifunga kutokana na ukosefu wa vyoo.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Juma Hamsini akiongea na Mwananchi Digital leo amesema shule hiyo ilifungwa Januari 25 mwaka huu.

Amesema choo kilititia na kingeweza kusababisha madhara kwa wanafunzi na halmashauri imenunua vifaa kwa ajili ya kupaulia.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Morotonga, Buruna Lucas amesema kila kaya inachangia Sh 16000 kwa ajili ya ujenzi huo.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz