Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi wa kike kupatiwa chanjo ya saratani shingo ya uzazi

52797 PIC+SOFIA

Wed, 17 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wadau wa chanjo mkoa wa Dar es Salaam wamekutana kujadili masuala mbalimbali ya afya ikiwamo uhamasishaji wa chanjo ya kujikinga na saratani ya shingo ya kizazi.

Lengo la mkutano huo ni kupata taarifa kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwamo watendaji wa manispaa na wa afya.

Mganga mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Yudas Ndungile leo Jumatano Aprili 17 amesema utoaji wa chanjo ya kuzuia saratani hiyo utahusisha wanafunzi wa kike wa shule za msingi na sekondari wenye miaka 14.

“Hatua hiyo ilianza mwaka jana ambapo tuliwachanja watoto 25,000 sawa na asilimia 93 na lengo letu mwaka huu tufikie asilimia 100,” amesema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sofia Mjema amesema chanjo hiyo ambayo itaanza kutolea Aprili 24 mwaka huu ni moja ya njia ya kujikinga na ugonjwa huo hatari unaowatesa wanawake.

Amesema maendeleo ya nchi yanaletwa na kizazi salama na chenye afya hivyo amewataka wazazi kuwahamasisha na kuwapeleka watoto wao kupata chanjo hiyo muhimu.

“Kuna ile dhana potofu kuwa mtu akichanjwa chanjo hii atakuwa mgumba, hii haina ukweli wowote chanjo hii imethibitishwa ni salama haina madhara kwa hiyo wazazi na walezi hakikisheni watoto wanapata chanjo hii.”

“Niwaombe pia wajumbe katika mkutano huo kujadili kwa kina na kuhakikisha kuwa majadiliano hayo yanaleta matokeo chanya katika mkoa wetu,” amesema.



Chanzo: mwananchi.co.tz