CHUO Kikuu cha Iringa kimelazimika kuwafukuza wanafunzi zaidi ya 50 baada ya kudukua mfumo wa malipo ya ada na kugoma kulipa ada ya kozi ya teknolojia ya habari (IT).
CHUO Kikuu cha Iringa kimelazimika kuwafukuza wanafunzi zaidi ya 50 baada ya kudukua mfumo wa malipo ya ada na kugoma kulipa ada ya kozi ya teknolojia ya habari (IT). Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Ndilirio Urio amesema wanafunzi 256 walifanya udanganyifu wa malipo na Chuo kiliagiza matokeo ya wanafunzi wote yafutwe. “Seneti ili kaa jana wale ambao wamekubali kulipa ada, kukiri na kuomba msamaha tumewasamehe,” amesema wakati wa mahojiano na waandishi wa habari. “Wale wachache waliokaidi kulipa wamefukuzwa.”