Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi UDOM kumkumbuka Magufuli mikopo elimu ya juu

Chuo Wanafunzi UDOM kumkumbuka Magufuli mikopo elimu ya juu

Thu, 25 Mar 2021 Chanzo: ippmedia.com

Suala la mikopo ilikuwa ni sehemu mojawapo ya kuchangia migogoro kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini iliyokuwa ikotokea mara kwa mara katika maeneo ya baadhi ya vyuo vikuu.

Akizungumza wakati wa mahojiano na vyombo vya habari Waziri wa Serikali ya wanafunzi wa UDOM James Mwaijambe, alisema mikopo ni sehemu muhimu kwa wanafunzi hususani anapokuwa chuoni akiendelea na masomo yake kwa sababu fedha hizo zinamsaidia katika matumizi yake ya kila siku.

"Mkopo kwa mwanafunzi ni muhimu sana kwa sababu inasaidia kuendesha maisha ya mwanafunzi anapokuwa masomoni,"alisema Mwaijambe

Amesema bila ya hivyo mwanafunzi hawezi kusoma kwa sababu atakwama kufanya mambo mengi ya msingi akiwa chuoni hapo.

Chanzo: ippmedia.com