Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi Mbeya wabuni drones za kusafirishia, kupulizia dawa

Drone Mizigooo.jpeg Drone

Sat, 23 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kimetengeneza ndege zisizo na rubani (drones) zitakazotumika kwa kazi 20 tofauti ikiwemo kusafirisha dawa na damu kutoka hospitali moja kwenda nyingine pamoja na shughuli za kilimo kama kumwagilia, na kupuliza dawa.

MUST kimeishukuru Serikali kwa kuendelea kuwekeza katika Miundombinu mbalimbali ikiwemo majengo na zana za kujifunza na kufundishia kwa kutoa fedha zaidi ya Shilingi Bilioni 40 kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia.

Akizungumza katika Maonesho ya 17 ya Vyuo Vikuu yanayofanyia katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam, kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo hicho Dickson Msakazi amesema kuwa fedha hizo zimekiwezesha Chuo hicho kujiimarisha katika maeneo mbalimbali ikiwemo miundombinu ya kitaaluma.

“Tunaishukuru Serikali kwa kutupatia fedha hizi ambazo zimefanikisha kufanya maboresho kwenye maeneo mbalimbali, ikiwemo vifaa vya kujifunzia, pale Chuoni tuna Maktaba kubwa ya kisasa yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi elfu 2500 kwa wakati mmoja yenye mifumo ya online, mwanafunzi anaweza kujisomea kupitia mtandao, hivyo halazimiki kushika kitabu”

“Pia, kwa sasa tuna maabara kubwa ya kisasa yenye uwezo mkubwa na inafanya uhandisi wa vifaa tiba, hivyo tunaishukuru sana Serikali” amesema Msakazi.

Amebainisha kuwa kwa sasa Chuo hicho kina wanafunzi elfu nane na kwamba kutokana na mpango wao wa miaka mitano Chuo hicho kitakuwa katika hatua nzuri zaidi na kuwa kati ya Vyuo Vikuu vikubwa hapa nchini na kuweza kudahili wanafunzi elfu tano

Chanzo: www.tanzaniaweb.live