Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi 963 washindwa kufanya mtihani kidato cha pili Njombe

IMG 20221125 WA0001 1 Wanafunzi 963 washindwa kufanya mtihani kidato cha pili Njombe

Fri, 25 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanafunzi 963 waliokuwa wanasoma kidato cha pili katika shule za sekondari mkoani Njombe wameshindwa kufanya mitihani yao ya kidato cha pili kwa mwaka wa 2022/2023 kutokana na utoro pamoja na sababu nyingine mbalimbali.

Afisa elimu mkoa wa Njombe Mwalimu Nelasi Mulungu ametoa taarifa hiyo katika kikao cha ushauri ya mkoa (KUM) kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe.

"Bado utoro upo,watoto 963 kwa mkoa mzima hawajafanya mtihani wa kidato cha pili,hawa walianza kidato cha kwanza vizuri lakini walipoingia kidato cha pili wakawa wamepotea kwasababu mbali mbali"amesema Nelasi Mulungu

Mulungu ametoa wito kwa wadau mbalimbali kushirikiana Ili kudhibiti vitendo vya utoro kwa watoto kwa kuwa wanakosa haki yao ya kupata elimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live