Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi 50,000 kupata vyeti vya kuzaliwa Geita

8970dcb695f2f8fa122cff302c3be177 Wanafunzi 50,000 kupata vyeti vya kuzaliwa Geita

Mon, 31 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAKALA wa Usajili U? lisi na Udhamini (RITA) umezindua zoezi la kuandikisha wanafunzi mkoani Geita wa umri wa kati ya miaka 5 na 17 na kuwapa vyeti vya kuzaliwa.

Mkakati huo umezinduliwa mwishoni mwa wiki na utatekelezwa katika wilaya ya Geita, ambapo kwa kuanzia wanafunzi 50,000 wanategemewa kusajiliwa na kupewa vyeti hivyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kaimu Mtendaji Mkuu wa RITA, Emmy Hudson alisema Halmashauri ya Wilaya ya Geita inaungana na wilaya nyingine 22 katika kutekeleza mkakati huo. “Mkakati umeanza vizuri

sana kwenye wilaya 22 za mwanzo ambapo idadi ya wanafunzi zaidi ya 368,000 wamesajiliwa na kupewa vyeti. Kwa wilaya ya Geita pekee tunategemea kutoa vyeti hivyo kwa wanafunzi wasiopungua 50,000,” alisema.

Aliitaja mikoa iliyofanikisha usajili huo kuwa ni Dar es salaam, Mara, Simiyu, Singida, Njombe, Ruvuma na Shinyanga. Usajili huo utahusisha mikoa yote na lengo ni kuhakikisha wanafunzi wote shuleni wanapata vyeti vya kuzaliwa.

Kwa mujibu wa Hudson, mwitikio wa wananchi katika kufanikisha usajili huo ni mkubwa. Ofisi yake inaendelea kubuni mbinu mbalimbali ili kufanikisha uandikishaji na utoaji wa vyeti kwa haraka.

Aliwataka wazazi kuchangia gharama kwenye zoezi hilo, linalogharamiwa na serikali kwa fedha za ndani, ambapo kila mzazi wa mtoto anatakiwa kuchanga si zaidi ya Sh 10,000.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita, Fadhil Juma aliwataka wakurugenzi wa halmashauri kuandaa mazingira mazuri kwa watumishi watakaoteuliwa kwenye usajili huo kushiriki bila kukosa kuhakikisha wanafunzi waliolengwa wanapata vyeti vya kuzaliwa bila usumbufu wowote.

Alisema utoaji vyeti vya kuzaliwa, unalenga kujua idadi ya watu katika nchi, akina nani, wanaishi wapi na wanafanya nini. “Huu ni mkakati mkubwa na kimsingi ni ulinzi na usalama wa nchi ili kuwatambua raia wake na kuwapa huduma stahiki.

Sio tu suala la idadi ya watu,” alisema. Uzinduzi huo ulienda sambamba na semina iliyowahusisha waratibu wa elimu kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, ambao walifundishwa mambo ya msingi yanayotakiwa kuzingatiwa wakati wa usajili wa wanafunzi na utoaji vyeti.

Waratibu hao watatoa mafunzo kama hayo kwa walimu wakuu au wasaidizi wao, watakaohusika na kazi za kila siku za usajili na utoaji vyeti hivyo kwa wenye sifa stahiki.

Viongozi wa dini waliahidi kusambaza ujumbe wa zoezi hilo kwa waumini wao. “Tuko bega kwa bega na serikali katika kuhakikisha zoezi la usajili na utoaji vyeti kwa wanafunzi wetu linafanikiwa na kuwa ajenda ya kudumu,” alisema Mchungaji John Ndaluka kutoka Umoja wa Makanisa ya Kikristo (CCT).

Chanzo: habarileo.co.tz