Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi 400 wanakaa chini Sengerema

Wanafunzi Chini Wanafunzi wakisomea chini

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: Mwananchi

Wanafunzi zaidi ya 400 wa darasa la nne na tano wanakaa chini na kutumia chumba kimoja cha darasa kwenye Shule ya Msingi Bugumbikiso iliyopo kata ya Chifunfu wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Paul Vicent amesema shule hiyo ina walimu 30 na wanafunzi 3, 118 kuanzia darasa la awali hadi la saba. Amesema sababu ya kukaa chini ni idadi kubwa ya wanafunzi licha ya Serikali kutoka Sh71 milioni kujenga vyumba vitatu vya madarasa na matundu 10 ya vyoo.

Mbunge wa Sengerema, Hamisi Tabasamu amesikitishwa na hali hiyo licha ya kutoka ushauri kuwa fedha hizo zitumike kujenga shule nyingine ili kuondoa msongamano huo.

Chanzo: Mwananchi