Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi 400 wahitimu chuo cha uganga wa jadi Kahama

Waganga 400(1) Wanafunzi 400 wahitimu chuo cha uganga wa jadi Kahama

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchi ya Tanzania limeingia katika vitabu vya historia kwa kutoa kundi la kwanza kabisa la wanafunzi ambao walikuwa wanasomea kozi ya uganga wa kienyeji.

Chuo cha Uganga wa Jadi cha Modesta kilichopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kimekuwa cha kwanza kabisa kutoa wahitimu wasiopungua 400 ambao walikuwa wanaandaliwa kwa mafunzo kabambe ya uganga wa kiasili.

Mahafali hayo yalihudhuriwa na umati wa watu Zaidi ya elfu moja kushuhudia kufuzu kwa wanafunzi hao ambao walipitia mafunzo ya uganga kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Mbunge wa jimbo la Kahama, Jumanne Kishimba alitoa wito kwa serikali kukumbatia mafunzo hayo ya asili akisema kuwa ni sehemu ya tamaduni na wala hakuna mila, destruri na tamaduni zilizo potovu.

“Sasa hivi kwenye mtaala mpya wa elimu, tunapeleka suala la utamaduni shuleni na mimi ndiye nilikuwa nalipigania sana kwamba jamani tunahangaika. Mjini tunasema sijui tunaugua msongo wa mawazo, matatizo ya akili, sasa mbona kijijini hawaugui huo msongo wa mawazo?

“Kwa nini tusiende kwao tukawauliza kama nyinyi hamuugui ina maana hizi dawa mnazo. Tunajaribu kwa njia zote kuendeleza mila sahihi,” mbunge huyo alisema.

Taifa la Tanzania kwa muda mrefu limekuwa likijulikana kwa mila ya uganga wa kiasili ambao wengi wanaumini na vile vile kuuambatanisha na matukio ya ushirikina na uchawi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live