Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi 22 wajeruhiwa na radi darasani

E6f4aebd7575506ce9ae281e81e8b5c0 Wanafunzi 22 wajeruhiwa na radi darasani

Wed, 2 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

ZAIDI ya wanafunzi 22 wa Shule ya Msingi De Paul iliyopo katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamejeruhiwa na radi wakiwa darasani.

Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Mgema amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mbali na wanafunzi pia mwalimu wa darasa hilo amejeruhiwa.

Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya, tukio hilo limetokea saa 8:00 mchana ambako idadi kubwa ya wanafunzi waliojeruhiwa ni wa darasa la sita na wachache wa darasa la tano.

Baada ya tukio hilo, uongozi wa shule hiyo ulifanya jitihada ya kuwapeleka Hospitali ya Rufaa ya Songea (Homso). Hata hivyo, wanaendelea vizuri.

Mgema alisema wanafunzi wengi wamepata majeruhi madogo na kwa wamelazwa kwa ajili ya kuendelea na matibabu na kutoa wito kwa wazazi kutoa elimu kwa vijana wao kwamba wanapoona radi sio vema kukimbilia chini ya miti ambako sio salama hasa katika kipindi hiki cha mvua zilizoanza kunyesha katika maeneo mengi nchini.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Songea, Dk Majura Magafu alisema watoto wote wanaendelea vizuri na wanapatiwa matibabu na kuwatoa hofu wazazi kwamba madhara ya radi yanakwisha taratibu.

Hii ni mara ya pili katika muda wa wiki moja kutokea tukio la radi ambako mwishoni mwa wiki iliyopita radi ilipiga katika Shule ya Sekondari ya Wavulana Songea ambako haikuleta madhara yoyote.

Chanzo: habarileo.co.tz