Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi 11,413 hawajaripoti shuleni Rukwa

Madarasa Ya Mil 520 Yakamilika Njombe, Yakabidhiwa Wanafunzi 11,413 hawajaripoti shuleni Rukwa

Fri, 3 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanafunzi 11,413 ambao ni asilimia 45 ya wanafunzi 25,362 waliotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza kwenye shule wa sekondari mkoani hapa hawajaripoti shuleni tangu shule hizo zilipofunguliwa Januari 9 mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Queen Sendiga amesema hayo Februari 2, 2023 wakati akitoa maelekezo kwa wakuu wapya wa wilaya katika wilaya za Sumbawanga na Kalambo.

Wakuu hao wa wilaya walioapishwa ni Dk Jane Nyamsenda ambaye atahudumu Wilaya ya Sumbawanga na Lazaro Komba aliyeenda Wilaya ya Kalambo.

Kufuatia kundi kubwa la wanafunzi kutokuripoti shuleni ameagiza kufanyika kwa masako wa nyumba hadi nyumba ili kuwabaini watoto ambao hawajaripoti shuleni ili waanze kwenda shule haraka iwezekanavyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live