Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wampongeza Rais Samia kwa kupata maji Iringa

P1012116 768x576 Wampongeza Rais Samia kwa kupata maji Iringa

Mon, 12 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi wa kijiji cha Ihomasa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa,wameipongeza Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(RUWASA), kwa kutekeleza na kukamilisha mradi ya maji ambao umemaliza kero ya upatikanaji wa maji safi na salama.

Wametoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti, wakati wakizungumza na Baadhi ya Waandishi wa Habari walioko kwenye ziara maalum ya kutembelea miradi ya maji inayotekelezwa na Ruwasa katika mikoa ya nyanda za juu kusini.

Walisema tangu Ruwasa ilipoanzishwa miaka minne iliyopita,wameshuhudia kazi kubwa na nzuri ya kutekeleza miradi ya maji katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Mufindi ikiwamo kijiji chao kilichopata mradi mkubwa wa maji ambao umekamilika kwa asilimia mia moja.

Mwenyekiti wa chombo cha watumia maji ngazi ya jamii(CBWSO) Monica Maluka alisema,kati ya mambo makubwa yaliyofanywa na wakala wa maji na usafi wa mazingira(Ruwasa)ni kukamilisha mradi huo.

Maluka alisema,tatizo la maji katika kijiji hicho lilikuwa kubwa na hivyo kuathiri sana shughuli nyingine za maendeleo kwani wananchi walitumia muda mwingi kwenda kutafuta maji kwenye vyanzo hasa mito midogo iliyopo kando kando ya kijiji hicho.

Kuhusu uchangiaji wa huduma ya maji alisema,awali kulikuwa na mwitikio mdogo wa wananchi kuchangia gharama za uendeshaji wa mradi huo,lakini baada ya kuelimishwa juu ya faida zake sasa mwitiko ni mkubwa.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji Aidan Kyando alisema,Ruwasa chini ya Mkurugenzi Mkuu Clement Kivegalo imefanikiwa kutekeleza dhamira ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani, kwani awali wananchi walilazimika kutembea kati ya km 2 hadi 3 kwenda kutafuta maji.

Alisema kuwa,mradi huo umesaidia kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa asilimia kubwa tofauti na hali ilivyokuwa huko nyuma na wananchi wameanza kutumia maji hayo kwa shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwamo kulima bustani za mboga.

Aidha alieleza kuwa,kukamilika kwa mradi huo kumemaliza matukio ya watoto wa kike kubakwa na kumaliza migogoro ya ndoa iliyojitokeza mara kwa mara hasa pale wanawake wanapochelewa kurudi nyumbani kutoka kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya familia zao.

Diwani wa kata ya Kasanga Coster Ng’umbi,mradi huo utachochea sana maendeleo ya kijiji cha Ihomasa na vijiji vingine vya kata hiyo kwani sasa wananchi watapata muda mwingi kujikita katika shughuli za maendeleo badala ya kwenda kutafuta maji mbali na makazi yao.

Ng’umbi, amewataka wananchi kutunza mradi huo na kuutumia kwa ajili ya shughuli zao za maendeleo kwani umetekelezwa ili kuwaondolea kero ya maji iliyokuwepo kwa muda mrefu.

Amewapongeza watendaji wa Ruwasa ngazi ya wilaya na mkoa kwa kukamilisha ujenzi wa mradi huo,lakini amewaasa kutobweteka na mafanikio waliyapata bali kuongeza uwajibikaji ili kupunguza zaidi kero ya maji kwa wananchi ambao bado wako kwenye mateso makubwa ya kukosa maji safi na salama.

Kwa upande wake Kaimu meneja wa Ruwasa wilaya ya Mufindi Irine Sengiwa alisema,mradi huo ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa kwa fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uvico-19 kwa gharama ya Sh.milioni 293,159,895.OO.

Alisema,mradi huo umelenga kuwanufaisha jumla ya wakazi 2,500 wa kijiji cha Ihomasa na umekamilika kwa asilimia 100 ambapo kwa sasa uko kwenye matazamio na unaendeshwa na chombo cha usimamizi na uendeshaji wa mradi(CBWSO.

Sengiwa alitaja mradi mwingine unaotekelezwa na Ruwasa ni katika kijiji cha Ulole ambao gharama yake ni Sh.milioni 214,861,605.00 na unahudumia zaidi ya wakazi 1,214 wa kijiji hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live