Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamiliki wa mabasi waliotuhumiwa na DC Sabaya wajisalimisha polisi

92539 Sabaya+pic Wamiliki wa mabasi waliotuhumiwa na DC Sabaya wajisalimisha polisi

Wed, 22 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Wamiliki wawili wa kampuni za mabasi yanayofanya safari zake kati ya Dar es Salaam- Arusha  waliotakiwa na mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya kujisalimisha polisi wametekeleza agizo hilo leo Jumanne Januari 21, 2020.

Wafanyabiashara hao, Clemence Mbowe wa Machame Safari na Rodrick Uronu wa Lim Safari wameripoti kituo cha Polisi Bomang’ombe wilaya ya Hai leo saa 3:00 asubuhi.

Wakati akikagua ukarabati wa reli ya Moshi-Arusha ili treni ya abiria inayotoka Dar es Salaam-Moshi kufika hadi Arusha, Sabaya aliwatuhumu wafanyabiashara hao kwa kuhujumu miundombinu ya reli.

Akizungumza katika kijiji cha Rundugai juzi Jumapili Januari 19, 2020, Sabaya aliwataka wafanyabiashara hao kuripoti polisi siku hiyo saa 12 jioni.

Licha ya kukanusha tuhuma hizo, wafanyabiashara hao walishindwa kuripoti polisi siku hiyo kutokana na sababu mbalimbali.

“Ni kweli mimi kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama nimejulishwa wamejisalimisha na wanaendelea kushikiliwa kwa mahojiano. Taarifa zaidi mtafuteni RPC (kamanda wa polisi wa Mkoa),”alisema Sabaya.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
DC Sabaya amesema jukumu lake lilimalizika alipotoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama, kwamba kwa sasa kazi ya uchunguzi inayoendelea ni wajibu wa polisi na vyombo vingine vya dola.

Chanzo: mwananchi.co.tz