Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamiliki wa IST wapewa tahadhari magari yao kuibiwa

JUMANNE MULIRO Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam , Jumanne Muliro

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: millardAyo

Jeshi la Polisi linaendelea na Operesheni maalum ya kukabiliana na Watu wanaojihusisha na wizi wa magari, zipo taarifa kuna kikundi cha Wezi kinacholenga kuiba magari aina ya IST.

Magari aina ya IST ambayo thamani yake ni milioni 11 hadi milioni 12 ambayo mifumo yake ya kiuendeshaji ni rahisi na hivyo kuweza kuibwa kirahisi.

“Tunaomba ushirikiano kwa Wananchi wote waendelee kutupa taarifa mbalimbali na wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu na Wahusika watakamatwa na tutazingatia ushahidi wa kisheria kuhakikisha Wahusika wanafikishwa Mahakamani” Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam.

Chanzo: millardAyo