Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamiliki ardhi wa awali Boko Dovya Kinondoni kulipwa fidia

5799 ANGELINA MABULA TZW

Thu, 5 Apr 2018 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI imezungumzia mgogoro wa ardhi eneo la Boko Dovya, wilayani Kinondoni na kusema utatuzi wake utatokana na wananchi waliovamia kuwa tayari kuchangia gharama za kurasimisha maeneo yao ili fedha zitakazopatikana zilipe fi dia kwa wamiliki halali.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anjelina Mabula alisema jana bungeni walishakaa vikao na wahusika kwa lengo la kuweka utaratibu utakaowezesha wamiliki wa awali (Somji) kulipwa fidia stahiki. Fidia hiyo inatakiwa ipatikane kwa fedha itakayopatikana kutoka kwa wananchi ambao watatakiwa kurasimisha maeneo waliyojenga ingawa Mabula alisema wananchi hawako tayari licha ya kwamba eneo si lao. Maelezo hayo ya Waziri aliyatoa wakati akijibu swali la Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) lililoulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Liwale, Zuberi Kuchauka (CUF).

Naibu Waziri alisema; “hata hivyo changamoto iliyopo katika kukamilisha makubaliano haya ni wananchi kupitia kamati yao waliyounda kutokuwa tayari kuchangia gharama za kurasimisha eneo hilo,” Alisema jitihada zaidi za wadau wengine akiwemo Mbunge wa Kawe, Mdee zinahitajika katika kuwaelimisha wananchi kupitia kamati yao kuwa tayari kushiriki katika upatikanaji wa ufumbuzi wa suala hili. Kwa mujibu wa Naibu Waziri, awali shamba hilo lililokuwa na ukubwa wa ekari 366 Mbweni maarufu kama Somji Farm, lilipimwa kwa upimaji Na.

E7/37F na kupewa namba ya upimaji 10917 ya Agosti 15, 1959 na kumilikishwa kwa Hussein Somji na Munaver Somji mwaka 1961 na baadaye kuandaliwa hati iliyosajiliwa kwa Na. 14573 ya kipindi cha miaka 99. Sehemu ya shamba hilo (ekari 8.5) zilitwaliwa kwa matumizi mahususi ya serikali mwaka 1975 na iliyobaki ilitwaliwa na serikali mwaka 2002 kwa ajili ya kutumika katika mradi wa viwanja 20,000.

Chanzo: habarileo.co.tz