Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliowekwa ndani kwa amri ya RC Mnyeti waachiwa

9464 MNYETI+PIC TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Babati. Polisi mkoani Manyara imewaachia huru watu watano akiwamo wakili wa kujitegemea ambao awali walikamatwa kwa kuwekwa mahabusu kwa amri ya mkuu wa mkoa huo, Alexander Mnyeti.

Watu hao waliokuwa wakishikiliwa kituo cha polisi Babati ni wakili wa jijini Arusha, Menrad De Souza na wafanyakazi wanne wa kampuni ya Barton, ambayo ni wakala wa pembejeo za kilimo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara,  Agostino Senga amewataja wafanyakazi wa kampuni ya Balton Ltd walioachiwa ni mhasibu wa kampuni ya hiyo Paul Sela, mhasibu msaidizi, Samwel Gambalila; ofisa utawala wa kampuni, Ummy Mwalimu na meneja utawala wa kampuni hiyo Pracksela Batemela.

Senga akizungumza na MCL Digital amesema watu hao waliachiwa jana Julai 31, 2018 na kwamba wanatakiwa kurejea katika kituo hicho baada ya wiki moja ili kujua hatima yao.

Soma Zaidi:

Mnyeti alivyowaweka ndani wakili, wateja wake

Wakili awekwa ndani kwa amri ya RC Mnyeti

Amesema watu hao walikamatwa Julai 30 kwa amri Mnyeti kwa kudaiwa kufanya uchochezi kwa kutumia mitandao ya kijamii, kuzua hofu na mtafaruku kwa jamii.

 

Mnyeti amesema aliagiza wakili huyo na watumishi hao wa kampuni ya Balton Ltd kukamatwa na polisi baada ya kusambaza ujumbe usio wa kweli kwenye mitandao ya kijamii kuwa amewafungia kwenye chumba na kufuli.

Chanzo: mwananchi.co.tz