Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliovamia Msitu wa Kuni watakiwa kuondoka

Waliovamia Msitu Wa Kuni Watakiwa Kuondoka Waliovamia Msitu wa Kuni watakiwa kuondoka

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewataka wananchi waliovamia Msitu wa Kuni na kuanzisha shughuli za ujenzi wa nyumba, kuacha mara moja na kuondoka katika eneo hilo la hifadhi .

Ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi katika Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.

“Sasa tunachowaomba kwanza kusimamisha ujenzi kwenye eneo la msitu, pili tutaangalia wale ambao wamejimilikisha maeneo makubwa lazima tuyagawe kwa sababu wote ni wavamizi,” amesisitiza Mhe. Masanja.

Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa huruma yake aliruhusu eneo la msitu limegwe jumla ya hekta 2000 ambazo zitagawiwa kwa wananchi lakini wananchi wameendelea kulivamia eneo la msitu.

“Mwaka jana tukaelekeza wananchi wapangwe kwenye hekta elfu 2000 na hiyo ni huruma ya Mheshimiwa Rais Samia kwanza naomba tumpongeze mama yetu ana huruma kwa sababu ilikuwa muondolewe lakini akasema hapana hawa ni wananchi wangu wapangwe,” Mhe. Masanja amefafanua.

Ameweka bayana kuwa wananchi waliomo kwenye hekta elfu 2000 zilzizogawiwa wako kihalali na watapimiwa ardhi na kupewa hati zao lakini waliovamia wanapaswa kuondoka katika eneo hilo.

Katika hatua nyingine , Naibu Waziri Masanja amewaasa wananchi wa Kijiji cha Ngombo Wilayani Malinyi, kuhifadhi mazingira na kuacha tabia ya kukata miti hovyo kwa faida ya kizazi cha sasa na cha baadae.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live