Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliosoma Azania sekondari waichangia shule hiyo madawati

25290 Azania+pic TanzaniaWeb

Sun, 4 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati makundi mengi ya WhatsApp yakitumika kama vijiwe vya kupigia stori, kundi la wanafunzi waliosoma shule ya sekondari Azania wamechangishana na kuisaidia shule hiyo.

Wanafunzi hao waliohitimu kidato cha nne mwaka 1992 wamekabidhi kwa uongozi wa shule hiyo viti na madawati 100 vyenye thamani ya Sh15 milioni.

Katibu wa umoja huo unaofahamika kama Azania Alumni, Abdi Abuu akizungumza wakati wa kukabidhi jana Ijumaa Novemba 2,2018 amesema wametoa msaada huo baada ya kubaini ni mojawapo ya changamoto inayoikabili shule hiyo.

Amesema walibaini kiwango cha elimu cha shule hiyo kimeshuka ndipo walipotuma wawakilishi wao kuzungumza na uongozi wa shule na uliowataarifu changamoto zinazowakabili ikiwemo upungufu wa madawati.

“Baada ya majibu hayo ndani ya kundi letu tukaanza kuhamasishana na tukakubaliana kuchangishana fedha na kununua madawati 100 ili kupunguza changamoto hiyo,” amesema.

Amesema msaada huo ni mwanzo wa mambo mengi ambayo wamepanga kuyafanya katika  shule hiyo kwa lengo la kuirudishia hadhi yake kwenye kiwango cha taaluma.

Chanzo: mwananchi.co.tz